MWANAMKE mmoja nchini Uchina ambaye ni mwanaharakati wa kutetea
wasichana kubaki bikra hadi waolewe, ametoa tangazo kwenye mtandao
akitafuta mume.
Mtandao wa rednet.cn umeripoti kuwa mwanamama huyo mwenye umri wa miaka
thelathini na nane aliandika tangazo hilo kwenye wavuti uitwao Sina
Weibo.
Mwanadada huyo anayejulikana kwa jina la Tu, aliandika vigezo anavyovitaka ambavyo mume huyo awe navyo.
Amesema lazima awe mwanachama wa chama kinachotawala nchini China, au
awe mfanyakazi wa serikali. Aidha amesema iwapo mchumba atapatikana,
hakutakuwa na tendo la ndoa kabla ya ndoa, na vile vile hakuta kuwa na
tendo hilo pia hadi miaka mitatu ya baada ya harusi.
Ujumbe huo wa Dada Tu, umezua sokomoko na kusomwa na zaidi ya watu elfu
kumi katika kipindi cha saa moja tu. Baadhi ya wachangiaji wa sakata
hilo wamesema kwa vigezo hivyo kamwe hatopata mchumba.
Kwa mujibu wa Mwanamama Tu ambaye anatokea jimbo la Hubei, amesema hana
muda tena wa kusubiri mchumba kwa njia za kawaida na ndio maana ametoa
tangazo hilo kwenye mtandao.


0 comments:
Post a Comment