ads

Habari Mpya

Friday, November 8, 2013

USIKU WA KHANGA ZA KALE 2013”, NI LEO NOVEMBA 8

 Asha Bilal
Na Andrew Chale
“LEO ndio Leo, lile Onesho la Usiku wa Khanga za Kale 2013, ‘Extra Vaa Khanga Party’  ndani ya  Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa ya Novemba 8.

 Katika onesho hilo, jioni ya leo, Mke wa wa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Asha Bilal anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kusindikiza usiku huo ambao pia utapambwa na mastaa mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, ikiwemo burudani murua kutoka kwa bendi ya Mashauzi Classic.

Mkurugenzi wa Fabak Fashion, Asia Idarous, ambao ndio waandaji wa maonyesho hayo, amesema tofauti na maonyesho mengine yaliyotangulia, Kanga ya Kale ya mwaka huu ina ladha tofauti kidogo ilikuwapa radha wadau wake..

“Licha ya kuonyesha matoleo mapya na mitindo ya kanga pia kuonyesha yale ya zamani ili kuleta vionjo zaidi kwa wavaaji wa sasa, tunakusudia kutoa darasa kuhusiana na thamani ya kanga japo kwa muda mfupi tu”, alisema.
 
Na kuongeza kuwa, usiku huo vazi la khanga ndilo litakuwa maalumu kwa wadau watakaohudhuria  sambamba na kupinga matumizi ya dawa za kulevya.

Kiingilio katika onyesho hilo ni sh 30,000 na viti maalumu itakuwa ni sh 50,000 ambako tiketi zinaendelea kuuzwa  Fabak Fashions Mikocheni na Gift Shop Serena Hotel pamoja na mlangoni  hapo hapo Serena hotel.
Aidha, usiku wa Khanga za Kale umedhaminiwa na Redd’s, CXC, Clouds FM, Vayle Spring, Magic FM, Eye View, Amina Design, Kabile, Voice of America, Origin Unite, Channel Ten, DTV, Times FM, Michuzi Media Group, Event Light na Miss Tanzania, New Africatv.com, Kajuna blog,Vijimambo blog  na wengineo kibao.

Maonyesho ya Kanga za kale nchini yanafanyika kwa mara ya tano tangu pale yalipoanzishwa rasmi mwake  mwaka 2008
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: USIKU WA KHANGA ZA KALE 2013”, NI LEO NOVEMBA 8 Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top