ads

Habari Mpya

Thursday, November 14, 2013

DK MWAKYEMBE AWACHARUKIA VIGOGO KATIKA IDARA YA POLISI, TRA NA BANDARI, NI WALE WANAOWASAIDIA WAFANYABIASHARA KUPITISHA MALI KATIKA BANDARI BUBU MKOANI TANGA.

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.


WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ametangaza vita rasmi na wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za magendo kupitia bandari bubu mkoani Tanga na maofisa wa vyombo vya Serikali waliopo kwenye mtandao huo.



Dk Mwakyembe aliwataka watambue kuwa, kiama chao kimefika kwa sababu tayari Serikali inayo majina ya wafanyabiashara na baadhi ya maofisa wa polisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA) wanaotumika kufanikisha upitishaji magendo.

Bandari ya Tanga.
 
Dk Mwakyembe ambaye aliwasili Tanga juzi na kufanya ziara ya ghafla kutembelea bandari bubu zilizoko mkoani hapa, alitangaza vita hiyo alipozungumza na maofisa wa TRA, polisi, TPA na wafanyabiashara.

Alisema baada ya Serikali kudhibiti Bandari ya Dar es Salaam, wafanyabiashara magwiji wa upitishaji bidhaa za magendo wamehamishia nguvu zao Tanga.

“Natangaza rasmi vita dhidi ya walio katika mtandao huo, watambue hatuwezi kuruhusu Bandari ya Tanga, bandari bubu na mpaka wa Horohoro kuwa gulio la walanguzi, wapitishaji dawa za kulavya na wahamiaji haramu,” alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: DK MWAKYEMBE AWACHARUKIA VIGOGO KATIKA IDARA YA POLISI, TRA NA BANDARI, NI WALE WANAOWASAIDIA WAFANYABIASHARA KUPITISHA MALI KATIKA BANDARI BUBU MKOANI TANGA. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top