ads

Habari Mpya

Saturday, November 16, 2013

HIKI NDICHO KIBIBI KIZEE KILICHOVUTA SIGARA LAKI 5 HUKU KWA SIKU KIKIVUTA SIGARA 15, KINA UMRI WA MIAKA 100.

DOROTHY HOWEDorothy Howe.

SUSSEX, Uinngereza
BIKIZEE wa umri wa miaka 100 ameibuka na kusema kuwa amevuta sigara laki tano tangu akiwa msichana mdogo.



Dorothy Howe ambaye ni katibu muhtasi mstaafu kutoka Uingereza alisema alianza kuvuta sigara tangu akiwa na umri wa miaka 16 na tabia hiyo ameendelea nayo hadi leo.


Alisema kwa kuvuta kwake sigara ametumia pauni 193,000 (zaidi ya sh. milioni 400) ambapo pia hutumia pombe kali aina ya whisky katika maisha yake.


Alipoulizwa kama ana mpango wa kuacha kuvuta sigara ajuza huyo alisema kuwa hataacha bali ataendelea na starehe yake hiyo hadi zipande bei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: HIKI NDICHO KIBIBI KIZEE KILICHOVUTA SIGARA LAKI 5 HUKU KWA SIKU KIKIVUTA SIGARA 15, KINA UMRI WA MIAKA 100. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top