Jifunze kuwa na kuongozwa na
malengo.
Mara nyingi
tumejikuta tukiwa kwenye mijadala na tukilalamikia umasikini wetu kusababishwa
na wazungu, nyimbo hizi zimeanza miaka mingi na kwa kadri tunavyozidi kulalama
ndivyo jinsi umasikini unavyo tuzidi siku baada ya siku. Tuna pumbazika tulilaani mabara ya ulaya na marekani kwa
kusababisha umasikini wetu wakati asilimia kubwa ya watu wa mabara hayo wapo
hapa kwetu miaka hii na wanazidi kufanikiwa kwa kutumia vilivyopo hapahapa na
isi tukiwa hapahapa tukiwatolea macho. Mtazamo wangu niwatofauti kidogo, na
ninaungana na baadhi ya tafiti ambazo zimebainisha kuwa tatizo letu kubwa
limekuwa sio sana
mtaji, ardhi au elimu bali ni Matumizi
mabaya ya muda, na Maisha yasiyokuwa na malengo.
Msingi wa
malengo yetu uwe kwenye kuwekeza katika ufanisi na kuweka kipaumbele kwenye
mafanikio yetu binafsi. Mipango mingi ya watu, hususan watu wa dunia ya tatu
imekuwa isiyohalisi na isiyoishia kwenye mafanikio maana haikuhusishwa na muda
muafaka , wenzetu wana msemo usemao“ No plan without Time span” yaani hakuna
mpango au lengo lisilo endana na muda.
Malengo
yamegawanyika katika makundi mawili, Malengo ya muda mrefu “Long term goals” na
malengo ya muda mfupi “short term goals”. Malengo ya muda mrefu ni ilemipango
ambayo inatuchukua muda mrefu kuitekeleza, kamavile ujenzi, elimu binafsi au ya
watoto, kutafuta mwenza wa maisha nk. Malengo ya muda mfupi ni ile mipango
ambayo tunaweza kuitekeleza kwa muda mfupi, kamavile kununua mavazi, kufanya
usafi, kuandaa sherehe nk. Mara nyingi inasemekana
kwamba malengo ya muda mrefu yanaweza kufikiwa kiufanisi ikiwa yale ya muda
mfupi yamekamilishwa vema.
Katika kuweka malengo marazote
jaribu kufikiria yafuatayo;
1. Nini
ninachotarajia kukifikia au kukipata katika lengo hili? “end product of your
goal”, usijiwekee lengo tu bila kupata picha ya matokeo. Picha ya matokeo
yanayoletwa na lengo hilo inamchango mkubwa sana katika kuchochea au
kudumaza ari yako kwenye kulifikia lengo
husika.
2. Ni
mikakati na rasilimali gani itakayo tumika katika kulifikia lengo husika. Wengi
hukaa kwenye vikao wakipanga mipango mingi ya kuanzisha miradi fulani bila
kuwaza juu ya mikakati na rasilimali zitakazotumika na mara tu wanapoanza
kutekeleza mipango yao hukutana na ugumu na ghafla husitisha mradi au
kuuahirisha kabisa. Wewe ni shahidi wa nyumba nyingi zilizoanzwa na kusitishwa,
Biashara nyingi zimefunguliwa kwa nguvu ya soda na ghafla kufungwa, watoto
wengi wamejikuta wakipelekwa shule Fulani walizoziona ni nzuri na gharama na
ghafla hawakumaliza mwaka wakahamishwa kukimbilia unafuu. Haya yote ni
mazingira ya watu wanaojaribu kuweka malengo pasipo kuangalia mikakati au
rasilimali zitakazo hitajika.
3. Niwatu
gani ambao nitawahitaji katika kulifikia lengo. Ni vizuri kujua kuwa kamwe
hatuwezi kufikia malengo yetu kwa kutegemea jitihada zetu wenyewe, iko sehemu
ambayo lazima utamwitaji mwingine. Wako waliojaribu kuanza mipango yao Fulani wakidhani
hawatamhitaji binadamu yeyote, mara uhitaji ukatokea na kukawa na ulazima wa
baadhi ya watu kuhusishwa, hapo ugumu mkubwa ukaanza. Ni vema kuishi na watu
vizuri maana hujui wapi utamhitaji nani kwa kusudi gani. Wako pia walioshindwa
kufikia malengo yao maana walifanya uchaguzi mbaya wa nani wa kumhusisha
malengo yao. Sio kila mtu ni mtu sahihi kuhusika katika lengo lako, wako ambao
unaweza kuwaambia tu waelewe nini kinaendelea na sio kushiriki, na pia wapo
ambao waweza kuwahusisha katika mchakato mzima. Ugumu unakuwa kwenye hekima ya
kuweza kutambua nani aelezwe pasipo kushiriki na nani aelezwe na kushiriki.
Unaweza ukafanya uchaguzi mbaya na ukawa na lengo zuri kabisa lakini
waliohusishwa wakaua lengo lako au kulitaifisha.
Itaendelea..........
IMEANDALIWA NA CHRISS MAUKI
MTAALAM WA SAIKOLOJIA NA JAMII (UDSM)
0 comments:
Post a Comment