ads

Habari Mpya

Monday, March 17, 2014

Exposed From Facebook......Unapokuwa Unataka Kuoa Zingatia Haya



Kwenye Maisha kuna Kila Siku ya Kujifunza kama utaamua kuwa Mwanafunzi Maishani. Moja ya Somo ambalo sikuwahi Kujifunza Kwenye Maisha Ni Maandalizi Ya Harusi. Nilikuwa Ninasikia tu zile purukushani za Kuandaa Harusi lakini sikuwahi Jua huwa inakuaje kuaje. Kwa Neema ya Mungu Mimi Nilipata Watu Wa Kuhakikisha sikondi wala Sipati Pressure. Bestman Wangu Mathew Mndeme na Mke wake Jacque Mndeme walihakikisha niko fiti hasa upande wa Saikolojia yangu ili nikiingia honeymoon kazi ni moja. 

Kamati yangu ya Maandalizi Chini ya Mwenyekiti Noell Tenga
makamu Kaleb Mwenda
Katibu Jasmine Harry James 
makamu Renee Lyatuu
Waweka Hazina Godwin ProtaceAnna-Abela Munyagi na Happyness Sasali Wa Lwendo Walihakikisha issue yoyote unayohusiana na harusi inabaki kuwa ya Kwao na sio ya Kwangu Ukweli ni Kwamba mpaka leo sijui walikusanya ngapi, tunadaiwa hatudaiwi walihakikisha nina baki kuwaza jambo moja tu, sio Vinywaji vimefanyaje, sijui Keki imeyeyuka hapana Waliibeba, Kamati nzima ilikuwa ni kama Wanafanya Kitu Chao Ila pamoja na yote Nilijifunza mambo yafuatayo ambayo ninadhani Maharusi Watarajiwa Prosper Alfred MwakitalimaPrezzor Fredy Chavala-The King,MC Pilipili Emanuel MathiasJoel MisesemoJames TemuRichard Chidundo na wengine woooote Wanaotarajia Kuoa na Kuolewa haya yafuatayo nimejifunza mimi na mengine nimeulizia watu wawili watatu kama na wao iliwatokea.

1. Usiweke Sana Tumaini lako Kwa Marafiki Isipokuwa Uwezo Ulionao. Katika Kipindi ambacho unaweza ukawashangaa unaodhani ni marafiki ni Kipindi cha Kuoa na Kuolewa. Kwenye akili zetu huwa tunadhani Wakati ambapo tunakuwa tunaoa na kuolewa Kila rafiki yetu atashobokea harusi yetu. Wakati wa Kuandaa Bajeti zetu unapiga mahesabu kuwa Kutokana na Mimi na Dr. Garvin Kweka tulivyo atachanga laki 3 akikosa kosa saaaana laki 2, tehe tehe dont try it at home ataku surprise atakapokuja kutoa Mchango wa fungu la kumi la laki 2 ambayo ni 20,000 atakutumia Tigo Pesa kisha atasema "Nimekutumia Japo uendee Salon" ukweli ni kwamba 20,000 sio pesa ila hukutarajia kama yeye atakuchangia 20,000 maana mkiendaga kwenye Kitimoto mnakula hadi 80,000 huku mkigombania Kulipa. Ukweli ni Kwamba nyakati na majira ya Kifedha kwa watu hazifanani unapopiga mahesabu yako kichwani ni heri ukapigia 0. Kisha andaa harusi yako ili ikitokea 10,000 ujue kabisa ni Muujiza, Kuliko Ukataraji 100,000 ikaja Buku 5 ya wembe utachanganyikiwa na mengi kisha unajikuta unaenda kwenye honeymoon una frustrations za kutosha halafu Binti anakushangaa mbona kama haufurahii honeymoon kumbe unawaza madeni baada ya harusi. Ajabu ni Kwamba Usio Wategemeaga Kwenye Issue za Harusi ndo huwa wanakuwa nawewe Mwanzo Mwisho wengine ulikuwa unawapa rate ya 50,000 unashangaa anakupa 1,000,000.

2. Kwa Wanawake Usitegemee Sana Marafiki Kukupa Support. Tofauti ya Wanaume wao iko kwenye Kuto Kupokelewa simu, Kuto kukusanya Michango Ila Kwa Wanawake sometimes ina athiri sana Mahusiano yao na Marafiki Zao na pengine na Ndugu Zao. Inapotokea marafiki zako Wote hawajaolewa wewe ndo umeolewa usitegee sana Kuwa watakupa support Mia Kwa Mia. Wengi Wata rudi nyuma kidizaini, ni kitu kinatokea bila wao kupenda itokee yaani ni kama wanakuonea wivu ni kama wanakuonea gere. Utashangaa wengine hata kauli zao zinabadilika utashangaa wanasema "mwenzetu una raha". Sasa usiombe Ulikuwa na shost wako wewe na yeye Wote Mliachwa na Wakaka, Ghafla Wa Kwako akarudi tena amerudi Kikweliii na amekuja Kuoa, aisee utaomba Poo. Mlikuwa mnaomba Wote, Mlikuwa mnalia Wote Ila utasikia "mbona Mungu amejibu kwako tuu". Ni hali ya kawaida ujiandae nayo Ukiwa unaenda Kuolewa utashangaa tu Siku ya Kitchen Party akawa Binamu yake anaumwa au Kazini kukawa Tight. Ukiwa kwenye Familia ambayo ina wadada wengi halafu wewe ni mdogo ndo unaolewa usitegemee sana vigelegele ukizingatia kuna dada zako wamegonga miaka 33 hawajaolewa. Utashangaa mambo mengi unafokewa fokewa kiajabu, mara unakatazwa sijui kuwasiliana siliana na Mumeo mtarajiwa, mara wanataka Uvae nguo ambayo wee huitaki Ukikataa Wanasusia kukupa Support Kwenye Send Off. Haya yatarajie ingawa sio katika familia Zote.


3. Kitu Kingine nimejifunza Matayarisho ya Harusi yana uhusiano sana na maisha yako unavyoishi na watu wengine. Kuna watu Harusi zao Watu wanajitolea mpaka basi, utashangaa mtu anasema ntakupa Suti,Ntakupa Viatu, Njoo uchukue shella, Niambie nini kimepungua, Kama gari la Maharusi Nakupa Benzi langu wewe weka mafuta, Nina Coaster hapa nyumbani njoo uchukue basi liwasaidie, Nitajitolea U-Mc mambo kadha wa kadha. Ukiangalia vizuri watu wa hivi ni Watu ambao wao wamekuwa wakijihusisha sana na mambo ya wengine. Inawezekana sio kifedha ila Ki hali wanajali sana Inter-Personal relationship yao na watu wengine. Kuna watu wanaishi kama wapo duniani na kuna watu wao wanaishi kama wapo Mbinguni. Vya wenzako wewe hujihusishi navyo, 'Uko Busy" usidhani vya kwako watu watashobokea na wao watakuwa "Busy" kuna harusi nimewahi Ona Sio ndugu wameibeba tu kama yao ila Marafiki Wameamua kuibeba kama yao. Unavyoishi na Watu duniani huwa ina matter sana kuliko unavyodhani. Kibinadamu kuna ile hali ya kuoneana aibu kuwa dhuu Jamaa alijitoa sana kwenye issue yangu. Hujawahi ona wewe unataka kupafanya kitu kidogo kwa ajili yako lakini Marafiki, Ofisi hata Kanisa wanasema "haiwezekani ufanye kitu kinyonge wewe ni mtu wetu sana, tutaibeba". Ninatambua kabisa watu tunatofautiana kwenye hulka zetu lakini hii haisababishi tusiwe wema kwa wengine. Biblia mbona inasema "Unavyotaka watu wakufanyie Wafanyie Wewe Kwanza.


4. Mnapoandaa harusi andaeni "Harusi Yenu". By the way Kiuhalisia Kabisa Harusi ni ya Mwanamke. Wanaume wachache sana Waliwahi kuwa na ndoto ya Harusi yao tofauti na wanawake ni siku waliyokuwa wakiisubiria sana. Ni Kitu kilichokuwa kwenye ndoto zao ni sehemu ya maisha yao. Sasa suala la Harusi kwa wadada linahusu nafsi, akili, roho na hisia. Ukitibua kimojawapo hapo ujue pameumana. Hakikisha kama umeandaa Surprise iwe +ve nimegundua hawapendi kuwa blind na siku yao, Kila kitu mashosti wanamuuliza Ukumbi wapi?aseme mmmh sijui Nguruka sijui PTA, Rangi sina hakika sana ila Blue and Black sijui, wanapenda wanapoulizwa waelezee Kikike hasa, they want to be part of It. Sasa wewe jifanye mjuaji ukalete Keki yenye maugali ugali utashangaa Mood ime change, Unashangaa Bibi Harusi amenuna unauliza nini anasema 'Bibi harusi alikuwa anata wimbo Wa Bon Mwaitege Sasa DJ ndo hana huo wimbo" sasa unashangaa Sasa Wimbo tuuu ndo akasirike vile??au wakati wa Kuombea sijui mwombaji alitamka maneno gani, basi yeye atakuuliza "umemsikia alivyoomba"??au MC sasa ukawa unacheza Nyimbo Bi harusi hazipendi. Nothing should happen kama Surprise yaani awe anapicha ya Ukumbi na Tukio mlilolitengeneza pamoja utaona tabasamu lake mwanzo Mwisho. Ulisema Mc atakuwa fulani anamuona pale, Muziki unapiga radha zenu, anawaona marafiki zako anawaona marafiki zake aliosoma nao anaofanya nao kazi kila kitu kinatokea anafurahia. Ukijifanya wewe Kidume na Familia yenu kuwa "Harusi ni Ya Mwanaume" basi ujue Ikisha Isha Sherehe ndo Utajua Harusi ya Mwanaume ama Harusi ni Ya Kwenu nyie Wawili Kila Mtu ameondoka mmebaki "Bwana Harusi na Bibi Harusi' ndo utajua Sherehe haikuwa ya Shangazi aliyetoa Milioni 2 ukamkubalia Kumleta Mc wake au keki ya Maunga Unga. Ukikosea Mguu Wa Kuingilia Kwenye Ndoa basi utakuwa na experience mbaya tangu siku ya Kwanza. 


credits to sammilembe
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Exposed From Facebook......Unapokuwa Unataka Kuoa Zingatia Haya Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top