ads

Habari Mpya

Friday, August 2, 2013

PATA KISA KAMILI CHA MREMBO CAROLINE CHA KUJIRUSHA KUTOKA GHOROFANI NA KUANGUKA CHINI KISHA KUDONDOKEA KICHWA, HUKO NCHINI ITALIA.


6



7
KAMPUNI ya mtandao wa kijamii wa facebook imezungumza baada ya tukio la yule msichana aliejiua kutokana na kisa ambacho kilianzia facebook January 2013.
Kumbe Chanzo ni picha ambayo ilikua inamuonyesha mrembo huyu wa Italia Carolina akiwa amelewa, aliiweka kwenye page yake ya facebook ambapo mpenzi wake wa zamani kwa kushirikiana na marafiki walianza kumtolea maneno machafu Carolina, walimtukana hivyo yeye na mdogo wake wa kike wakaamua kuripoti facebook lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Kwenye mji wa Italia wa Novarra ndio tukio lilitokea kupitia facebook na likaingia mpaka kwenye maisha ya Carolina ambapo bila yeye kujua, tukio liliendelea kuwa kubwa na kutishia kuwa kubwa kumshinda.
2
Kati ya saa tisa au nane usiku Carolina alijirusha kutoka kwenye dirisha la chumbani kwake gorof
ani nyumbani kwao na akaangukia kichwa, kichwa ndio kilitangulia kutua kwenye sakafu ya zege ambapo baada ya kufariki ilipatikana barua aliyoiandika maalum kwa wanaomtesa…. aliandika ‘“mmefurahi sasa ?  mmeniumiza vya kutosha? mmepata kisasi mlichokuwa mnatafuta ?“
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba mwendesha mashtaka Mahakamani Novarra anaangalia uwezekano wa kuishtaki kampuni ya facebook kwa kushindwa kuziondoa kauli chafu zilizokua zimeandikwa kwenye wall ya Carolina ambazo ndio zilipelekea kujiua.

1
4
5
Hata hivyo facebook wamezungumza kuhusu hicho kifo kwa kusema “tumesikitishwa na tukio la kifo cha Carolina, mioyo yetu na mawazo yetu yako kwa familia yake na marafiki zake, unyanyasaji wa aina yoyote ile hauna nafasi kwenye facebook na siku zote tumekuwa tukiwasisitiza vijana na wazazi kutoa ripoti za matukio kama haya, tunatoa maneno yote ambayo yanaenda kiunyume na sheria na sera yetu”
3
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: PATA KISA KAMILI CHA MREMBO CAROLINE CHA KUJIRUSHA KUTOKA GHOROFANI NA KUANGUKA CHINI KISHA KUDONDOKEA KICHWA, HUKO NCHINI ITALIA. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top