ads

Habari Mpya

Saturday, November 16, 2013

HIVI NDIVYO MWILI WA MAREHEMU DK.SENGONDO MVUNGI ULIVYOPOKELEWA KWA MAJONZI JANA USIKU JIJINI DAR ES SALAAM.


Wanachama wa NCCR-Mageuzi wakiwa wamelibeba sanduku lililohifandhi mwili wa kiongozi huyo wa NCCR-Mageuzi na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.


Mwili wa Marehemu Dk. Sengondo Mvungi ukifanyiwa maombi mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana usiku.

Waombolezaji waliofika uwanjani hapo kuupokea Mwili wa Dk. Mvungi.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiwa uwanjani hapo.

Baadhi ya waombolezaji waliofika uwanjani hapo.

Mjane wa Marehemu, Bi Anna Mvungi akiwa uwanjani hapo kuupokea mwili wa mumewe


Ndugu wakilia kwa uchungu.


Na Father Kidevu.
Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Marehemu Dk. Sengondo Mvungi umewasili nchini kutoka Afrika Kusini.


Makumi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu dk. Sengondo Mvungi walifika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere upande wa Mizigo na kuupokea mwili wa kiongozi huyo na mwana familia.


Mapokezi ya mwili wa Dk. Mvungi aliyefariki juzi kufuatia majeraha ya shambulizi la majambazi lililomkuta nyumbani kwake nombemba 2 mwaka huu na kupeleka Nchini Afrika Kusini kwa Matibabu, yaliongozwa na Mkewe mama Anne Mvungi.


Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Sengondo Mvungi, Mwenyekiti wa NCCR-Magezi, na wajumbe takriban wote wa tume ya mabadiliko ya Katiba mpya.


Sanduku hilo lilifunikwa bendera ya Chama cha NNCR-Magezi.

Mwili wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi unaagwa leo katika viwanja vya Karimjee kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini Kwao Kisangara juu, Wilaya ya mwanga mkoani Kilimanjaro kwa Maziko siku ya jumatatu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: HIVI NDIVYO MWILI WA MAREHEMU DK.SENGONDO MVUNGI ULIVYOPOKELEWA KWA MAJONZI JANA USIKU JIJINI DAR ES SALAAM. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top