USO
ni sehemu ya kuonyesha uhalisia kwa mwanamke na unapotaka kujua ni jinsi
gani mwanadada au mwanamke anapenda urembo basi utamwangalia usoni.
Kwa
mtazamo huo utaona yule mpenda urembo akiwa amepaka baadhi ya vipodozi
usoni kwa mfano:- Poda, Lip-Stick, Wanja n.k na utagundua kwamba
niliyekutana naye ni mmoja kati ya wanawake wanaopenda urembo.
Leo imekuletea mada ya jinsi unavyoweza kusafisha uso wako na ili uelewe hilo fuata haya yafuatayo:-
a)Penda kuosha uso wako kwa maji safi na salama na ili kujiepusha na mlipuko wa maradhi yatokanayo na maji.
b)Kama uso wako wa mafuta basi tumia maji yenye uvugu vugu, ili
kupunguza mafuta usoni mwako na ili kuuwezesha uso kuwa mkavu na kama
unasura isiyo kavu, basi nakushauri utumie maji yoyote unayopenda kama
ni vugu vugu au ya kawaida.
c)Tumia sabuni yoyote nzuri uitumiayo kunawia uso wako siku zote, ili kuiboresha ngozi ya suo wako.
d)Ila penda kutumia sabuni zisizo kali pindi usafishapo uso wako na
itakuepusha na baadhi ya matatizo ambayo wanawake wengi huyapata kwa
utumiaji wa sabuni kali.
e)Tumia kitambaa safi na salama au taulo laini lililosafi na salama ili usipate matatizo ya michubuko usoni mwako, kitu kitakachopelekea kutokuwa na ngozi nzuri usoni.
f)Usipende kutumia kilevi cha aina yoyote na kama ni mtumiaji usitumie
kupita kiasi, kwani itapunguza uzuri wa sura yako kwani ulevi siku zote
ni mbaya hupunguza baadhi ya vitamins mwilini mwa mwanadamu.
g)Pia usipende kutumia sigara si nzuri kwa uboreshaji wa sura yako na afya yako kwa ujumla.
h)Jitahidi usiwe mtu wa kutoka toka sana usiku ili upate muda mrefu wa
kupumzika na uzidi kuboresha na kuirutubisha ngozi ya uso wako na
kuifanya ipendeze daima.
i)Pia unashauriwa kunywa maji, kula mboga za majani na matunda kwa
wingi, na kwa kufanya hivyo utazidi kuonekana ni mwanamke mwenye sura
safi, nyororo na iliyo na afya njema na yenye kuvutia daima machoni mwa
jamii inayokuzunguka.
kwa hisani ya manyandahealthy.
0 comments:
Post a Comment