MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Robin
van Persie amesherehekea miaka 30 ya kuzaliwa kwake leo, na mpishi wa
klabu alitoa mchango wake.
United imetweet picha ya keki
iliyotengenezwa na mpishi wa klabu kwa ajili ya Van Persie, ikiwa na
ujumbe usemao; 'Happy Birthday' katika lugha ya Kiholanzi.
Mapema, klabu pia ilichangia bago la 'RVP' kwa heshima ya mfun gaji wao huyo bora msimu uliopita kutimiza miaka 30.
Van Persie alifunga mabao 31 United msimu uliopita baada ya kuhamia akitokea Arsenal.

Kwako, Robin: Mpishi wa United ameonyesha keki aliyomtengenezea Robin van Persie, ikisema 'Happy Birthday' Kiholanzi

Furahia kuzaliwa: Manchester United imetweet picha hii ya Van Persie akitimiza miaka 30 Jumanne

Matawi ya juu: Van Persie alikuwa mfungaji bora wa United msimu uliopita kwa mabao 31
Wakati huo huo, wakati United ikijiandaa
na mchezo wake ujao na Stockholm, Nani na Bebe wanatarajiwa kuukosa
mchezo huo baada ya kucheza mpira wa meza.
Mabingwa wa England wapo Sweden kwa
ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya AIK Fotboll leo usiku, na Nani na
Bebe walikuwa wakicheza mpira wa meza katika hoteli ambayo timu imefikia
Stockholm.
Kikosi cha David Moyes kimeshinda mechi
mbili tu katika mechi tano za kujiandaa na msimu kwenye ziara yake ya
Asia na Australia.
United ilifungwa 1-0 na Singha All Stars Julai 13 na wakafungwa tena Yokohama F-Marinos 3-2.

Kichwa kwa kichwa; Nani (kushoto) akicheza na mchezaji mwenzake Bebe (kulia) mpira wa meza
Lakini ushindi wa 5-1 dhidi ya A-League
All Stars na 5-2 dhidi ya Kitchee ulirejesha matumaini kwamba United
bado ina safu ya nguvu ya ushambuliaji iliyowawezesha kuweka rekodi ya
kutwaa taji la 20 msimu uliopita.
Vijana wa Moyes walihitimisha mechi zao
za kujiandaa na msimu kwa mechi ya kumuaga Rio Ferdinand usiku wa Ijumaa
Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Sevilla kabla ya kumenyana na Wigan
katika mechi ya Ngao ya Jamii Jumapili.
Kampeni ya kutetea taji lao inaanza Jumamosi, Agosti 17 na Swansea ugenini.
0 comments:
Post a Comment